ALSHIFAA FC MABINGWA WA SISI NI DOLA CUP
Alshifaa FC wametawazwa mabingwa wa michuano ya SISI NI DOLA CUP – Makala ya Pili, baada ya kuichapa Green Eagles mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwa ushindani mkubwa.
Alshifaa walipata bao la kuongoza dakika ya 24 kupitia kwa Lawrance Dady, kabla ya Mohamed Juma kuongeza bao la pili dakika ya 50 na kuwapa Alshifaa FC mkwaju mpana kuelekea ubingwa.
Green Eagles walipata bao la kufutia machozi dakika ya 74 kupitia kwa Mohamed Yanga, aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, lakini juhudi zao za kusawazisha hazikuzaa matunda hadi filimbi ya mwisho.
Kwa ushindi huo, Alshifaa FC wamejinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja, pamoja na medali. Green Eagles, waliomaliza katika nafasi ya pili, wamepata shilingi laki tano na medali, huku Azam FC, waliomaliza nafasi ya tatu, wakiondoka na shilingi laki mbili na nusu pamoja na medali.
Katika tuzo binafsi, Nassir Hassan wa Alshifaa FC ametwaa tuzo ya Kocha Bora wa Michuano, huku Lawrance Okoth wa Alshifaa akichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Michuano. Tuzo ya Kipa Bora imekwenda kwa William Mandada wa Green Eagles.
Tuzo ya Wafungaji Bora imegawanywa kati ya Joshua Oyoo wa Fayaz Bakers na Enock Lemeyian wa Juve FC, ambao wote walifunga mabao matano. Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi imekwenda kwa Ahmed Hussam Di Maria wa Mombasa Kings.
Hawa hapa Lawrance Okoth mchezaji Bora WA michuano hiyo MVP amesema kupitia juhudi zake na timu yake imemuwezesha kupata Yuzo hiyo nae Ahmed Di Maria mchezaji chipukizi wa michuano hiyo ameelezea furaha yake baada ya kutwaa tuzo hiyo akisema kupitia wachezaji wenzake ambao Wana uzoefu wamemuwezesha yeye kungara uwanjani akisifia Dola Kwa kuandaa michuano hiyo ambayo inatoa fursa Kwa vijana wadogo.
Mkufunzi wa Alshifaa FC, Nassir Hassan, amesema mchezo wa fainali haukuwa rahisi, lakini vijana wake walijituma na kutumia vyema nafasi walizopata na hatimaye kuibuka na ushindi. Amesema michuano hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuibua, kutambua na kukuza vipaji vya vijana.
Kwa upande wao, viongozi wa maandalizi ya michuano hiyo wamesema mashindano yamefanikiwa kwa kutoa jukwaa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao, huku baadhi yao tayari wakipata fursa za kwenda kufanya majaribio katika timu za ughaibuni.
Viongozi hao wameongeza kuwa kupitia michuano hiyo, wameunda kikosi maalum kitakachocheza mechi za kirafiki jijini Nairobi, hatua inayolenga kuwapa vijana nafasi zaidi ya kuonyesha uwezo wao na kujitangaza katika soka.
Comments
Post a Comment