DEREVA WA LORI AJISHINDIA SHILINGI MILIONI 102 KATIKA SPORTPESA MEGA JACKPOT
Na Hafsa Juma Dereva wa lori mwenye umri wa miaka 47, Peter Mwaniki Maina, amejishindia kitita cha shilingi milioni 102 kupitia shindano la SportPesa Mega Jackpot baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi zote 15. Mwaniki, ambaye ni baba wa watoto wanne na amekuwa akifanya kazi ya udereva wa malori kwa takriban miaka 20, amesema ushindi huo utampa fursa ya kuboresha maisha ya familia yake na kuimarisha ustawi wao wa kifedha. Akizungumza wakati wa kutambulishwa rasmi kwa mshindi huyo mjini Mombasa, Mwaniki alisema hana mpango wa kufanya maamuzi ya haraka kuhusu matumizi ya fedha hizo, akisisitiza kuwa anahitaji muda wa kutafakari kabla ya kuamua hatua za kuchukua. “Kwa sasa sina mipango yoyote ya haraka kuhusu matumizi ya fedha hizi. Nimepata ushindi huu bila kutarajia, hivyo sitaki kufanya maamuzi ya pupa. Nitaendelea na kazi yangu ya udereva huku nikitafakari kwa kina kuhusu hatua nitakazochukua,” alisema Mwaniki. Kwa upande wake, Afisa wa Mawasiliano wa SportPesa, W...