Katana Aivusha Nyundo FC Nusu Fainali, michuano ya SISI NI DOLA CUP ikipamba Moto


Tuangazie matokeo ya Ngarambi za dimba ;la SISI NI DOLA Cup ambapo Mechi ya pili ya hatua ya robo fainali umewakutanisha Nabadda FC dhidi ya Nyundo FC katika pambano lililojaa mhemko mbwembwe na ushindani mkubwa.

Nyundo FC walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema kupitia kwa Joash Ndela katika dakika ya 4 kipindi cha kwanza. Hata hivyo, Nabadda FC walirejea mchezoni baada ya Ahmed Mohamed kujifunga kwa bahati mbaya katika dakika ya 21, na kufanya matokeo kuwa sare ya bao 1-1 hadi mwisho wa dakika 90 za kawaida.

Hata hivyo mshindi ameamuliwa kwa mikwaju ya penalti, ambapo Nyundo FC walionyesha utulivu na umakini mkubwa, wakishinda kwa mikwaju 4-2 dhidi ya Nabadda FC.

Francis Katana mlinda lango wa Nyundoi FC ndiye aliyekuwa nyota na moto wa kuotea mbali kwa kuokoa mikwaju 2 ya penalty, akibaini kuwa umakinifu wake na kujiamini katika mikwaju ndiko kumemwezesha kuip timu yake ushindi.
Mpaka Sasa Francis Katana wa Nyundo FC ndie kipa bora akiwa na michezo minne bila kufungwa akionyesha kiwango Cha juu katika michuano hayo.


Naye kocha wa Nyundo FC Swaleh Abdallah SUNDA ameeleza kuwa mechi hiyo haikuwa rahisi kama ilivyotarajiwa kwani timu zote 2 zilikuwa nzuri na zenye maandalizi kabambe huku akimpongeza kipa wao kwa kupangua mikwaju ya penalty akisema kuwa walikuwa wamejiandaa kwa mikwaju hiyo.

Sunda ameahidi kuwa watazidisha maandalizi katika hatua zijazo ili wapige hatua kubwa zaidi ya kufika fainali.

Kwa ushindi huo, Nyundo FC sasa wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya SISI NI DOLA CUP na watakutana na Green Eagles ambao waliwatitiga Likoni United goli 4 bila jibu katika robo fainali ya kwanza, mechi hii ikitazamiwa kuwa moto wa kuotea mbali.

Hapo kesho Ijumaa robo fainali nyingine itakutanisha AL-SHIFAA dhidi ya Mombasa Sports club.

Comments

Popular posts from this blog

Where Waste Becomes a Livelihood

Kwale Women Seek Bigger Voice in Coastal Fisheries and Blue Economy.

Kenya Power Celebrates Customer Service Gains as Kwale Customer Base Hits 106,000.