DEREVA WA LORI AJISHINDIA SHILINGI MILIONI 102 KATIKA SPORTPESA MEGA JACKPOT
Na Hafsa Juma
Dereva wa lori mwenye umri wa miaka 47, Peter Mwaniki Maina, amejishindia kitita cha shilingi milioni 102 kupitia shindano la SportPesa Mega Jackpot baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi zote 15.
Mwaniki, ambaye ni baba wa watoto wanne na amekuwa akifanya kazi ya udereva wa malori kwa takriban miaka 20, amesema ushindi huo utampa fursa ya kuboresha maisha ya familia yake na kuimarisha ustawi wao wa kifedha.
Akizungumza wakati wa kutambulishwa rasmi kwa mshindi huyo mjini Mombasa, Mwaniki alisema hana mpango wa kufanya maamuzi ya haraka kuhusu matumizi ya fedha hizo, akisisitiza kuwa anahitaji muda wa kutafakari kabla ya kuamua hatua za kuchukua.
“Kwa sasa sina mipango yoyote ya haraka kuhusu matumizi ya fedha hizi. Nimepata ushindi huu bila kutarajia, hivyo sitaki kufanya maamuzi ya pupa. Nitaendelea na kazi yangu ya udereva huku nikitafakari kwa kina kuhusu hatua nitakazochukua,” alisema Mwaniki.
Kwa upande wake, Afisa wa Mawasiliano wa SportPesa, Willis Ojwang, alisema kampuni hiyo itamunganisha mshindi huyo na wataalamu wa masuala ya fedha ili kumsaidia kupanga matumizi na kusimamia vyema fedha alizojishindia.
Ojwang alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa ushindi huo unaleta manufaa ya muda mrefu kwa Mwaniki na familia yake.
“Nia yetu ni kuhakikisha kuwa fedha hizi zinamnufaisha Mwaniki pamoja na familia yake. Kuanzia wiki ijayo, tutamunganisha na wataalamu wa masuala ya fedha watakaomshauri namna bora ya kuzisimamia na kuzitumia fedha hizo,” alisema Ojwang.
Mwaniki ndiye mshindi wa kwanza wa zawadi kuu ya SportPesa Mega Jackpot mwaka huu. Wakati huo huo, Caroline Nyakundi na Gaudencia Sella walijishindia bonasi za shilingi milioni 2.19 na milioni 3.5 mtawalia.
SportPesa Mega Jackpot ni shindano la kubashiri matokeo ya mechi za soka, ambapo washiriki hupewa fursa ya kujishindia zawadi kubwa kwa kutabiri kwa usahihi matokeo ya mechi zote 15 zinazoshindaniwa.
Comments
Post a Comment