Posts

USIMAMIZI WA BASETITANIUM WAJITENGA NA MADAI YA KUAHIDI KULIPA MILLION 7 KWA SHIRIKA LA KIJAMII LA SPORTS FOR ALL

Image
wafanyikazi wa shirika la kijamii la sports for all Usimamizi wa kampuni ya uchimbaji madini ya basetitanium umejitenga na madai ya kueneza ukabila ,ahadi za uongo na utumizi mbaya wa afisi yaliyoibuliwa na shirika la kijamii la michezo la Sports For All, ukiyataja madai hayo kukosa msingi na yanalenga kudhalilisha usiamamizi wa kampuni hio wakati inapojiandaa kufunga virago vyake mwishoni mwa mwaka huu . Wafanyikazi wa Shirika la sports for all wanalalamikia kutolipwa mishahara yao ya miezi mitatu ya shilingi milioni 3 ya mwaka 2018 mbali na shilingi milioni 7 ya mkataba wao uliokamilika mwezi June. wafanyikazi wa shirika la kijamii la sports for all Kadhalka wakidai kuwa usimamizi wa basetitanium umedinda kuwapa vifaa walivyokuwa wakifanyia kazi ikiwemo laptops ,printers ,files miongoni mwa vifaa vyenginezo. Wanaitaja hatua hio kukiuka haki zao ,hivyo kutaka usimamizi wa basetitanium kutimiza ahadi zao ikizingatiwa kuwa wamefanya kazi kwa ushirikiano kwa muda wa miaka kumi sasa. Mane...

SPIKA WA BUNGE LA KWALE AKANUSHA MADAI YA UTEPETEVU.

Image
                                            bunge la kaunti ya Kwale. Habari:Caroline Katana.  Spika wa bunge la kwale Seth Mwatela Kamanza ametetea afisi yake dhidi ya madai kuwa amewaeka bungeni wajumbe wateule watano kinyume cha sheria ,akiyataja madai hayo kuwa yenye kupotosha na kudhalilisha afisi yake kwani watano hao wamo bungeni kufuatia agizo la mahakama. Kesi dhidi ya wajumbe hao wateule iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa mjumbe mteule Mary Kalinga ,kwa kile alichokitaja kuwa uteuzi wao ulifanywa kwa njia isiyokuwa halali. Kamanza akiafiki kufahamu kesi inayowakabili wajumbe hao japo kusema kuwa hana mamlaka ya kuwatoa bungeni baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kuendeleza majukumu bungeni humo hadi pale kesi dhidi yao itakapotolewa uamuzi . Amehoji kuwa baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kusimamishwa kwao mnamo tarehe 14 mwezi September mwaka jana ,watano h...

AFISI YA DCI KINANGO YALAUMIWA KWA KUMUUNGA MKONO TAPELI WA ARDHI YA JAMII YA KURANZE.

Image
wakaazi wa Kuranze katika mkao na Mwakilishi wadi ya Puma.  Taarifa yake : Caroline Katana Sitoruhusu mtu yeyote kuwadhulumu wakaazi haki yao ya umiliki wa ardhi katika kipindi changu cha uongozi . Hii ni kauli ya mwakilishi wa wadi ya Puma aliyepia mwenyekiti wa bunge la kaunti ya Kwale James Dawa . Kauli yake inajiri baada ya mwenyekiti mdogo wa jamii ya wachimbaji migodi huko kuranze eneo bunge la kinango Hamisi Dena Mdoe kuanzisha mchakato wa kupiga bei ardhi ya jamii ya Kuranze yenye takriban hekari elfu 69.45 kinyume cha sheria. mwakilishi wa wadi ya puma James Dawa Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari baada ya kikao na jamii ya wafugaji, wachimbaji migodi nawafanyibiashara katika kijiji cha Kuranze , bw.Dawa ameafiki hadi kufikia sasa jumla ya watu 230 kutoka kaunti tofauti tofauti humu nchini kuuziwa ardhi hio na bw.Dena “ Niko na orodha ya watu 230 ambao tayari wameuziwa hekari 50 kwa shillingi 1,500 kila mmoja na hakuna hati miliki wanayopewa ,hii ni hali ya kushangaza sa...

KAYA TIWI GIRLS BASKETBALL TEAM TO DEFEND EAST AFRICA CHAMPIONSHIP IN MBALE, UGANDA.

Image
Matuga member of the parliament flags-off Kaya tiwi girls basketball team By Caroline Katana Basketball is one of the most popular sports played widely in Africa ,it is the second most popular sports in the continent next only to football . It is most prevalent in countries like Nigeria ,Egypt ,Tunisia ,Ivory coast ,Senegal ,etc. Figures such as Hakeem Olajuwon and Dikembe Mutombo have played an instrumental role in developing and popularizing basketball in the continent . Africa has produced some of the finest basketball players to date and has paved the way for other countries to participate internationally in the sport . The rich history of basketball in Africa is filled with great players and organizations striving to take this sport to another level . These sports have encouraged and empowered many athletes from around the world to play in professional leagues . Basketball has allowed athletes from Africa and places around the world to make a name for themselves and their countrie...

SPIKA WA BUNGE LA KWALE ATAKIWA KUTII AGIZO LA MAHAKAMA

Image
Mwanabiashara Richard Onsongo  Taarifa yake : Caroline Katana  Baadhi ya wakaazi kaunti ya Kwale wameishtumu vikali hatua ya bunge la kaunti hio kwa kuendelea kuwahifadhi na kuwalipa mishahara na marupurupu wawakilishi wadi wateule watano ambao uteuzi wao uliharamishwa na mahakama kuu ya Mombasa mnamo tarehe 14 mwezi Septemba mwaka jana . Kesi ya watano hao iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa mtawadi mteule Mary Kalinga mwaka 2023 baada ya kubainika kuwa waliteuliwa kinyume cha sheria .   Kwa miezi miwili sasa wamekuwa wakietekeleza shughuli za bunge na kupokea mishahara na marupurupu katika mazingira yasiyoeleweka . Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari huku Diani kaunti ya Kwale , mwenyekiti wa Chama cha Uzalendo nchini Richard Onsongo amesema kuwa watano hao walijaribu kutafuta usaidizi katika mahakama ya upeo ambapo pia juhudi zao ziliambulia patupu mwezi Machi mwaka huu , hivyo kushangazwa jinsi afisi ya spika wa bunge la Kwale Seth Kamanz...

KESI 300 ZA MAKACHERO BADIA WA EACC ZA RIPOTIWA.

Image
Eric Ngumbi  Habari : Shokah Juma kwale.  Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imesema kwamba katika mwaka wa 2024 pekee, imepokea kesi 300 za matapeli wanaojifanya kuwa maafisa wa EACC na ambao wamekuwa wakiomba rushwa kutoka kwa maafisa wa serikali kuu na za kaunti, wakuu wa shule, na wamiliki wa biashara binafsi wakidai kuwa wanachunguza tuhuma dhidi yao. Akizungumza huko Diani, Kaunti ya Kwale, msemaji wa EACC Eric Ngumbi alisema kuwa matapeli hao wamekuwa wakidai pesa ili kuwaondolea waathiriwa madai ya kesi za ufisadi ambazo hazipo. Hii inafuatia kukamatwa kwa washukiwa watano huko Kitui waliovamia nyumba ya Mkurugenzi wa Mapato wa Kaunti ya Kitui na kudai rushwa kutoka kwake wakidai kwamba anahusika katika kesi ya ufisadi. EACC inasema kwamba washukiwa hao pia wanaendesha ofisi haramu katika kaunti wakijifanya kuwa mawakala wa tume.

NANI ATAZIOKOA ARDHI ZILIZONYAKULIWA TIWI ?

Image
  Wakaazi mahakamani mjini Kwale Taarifa yake: Caroline Katana Katika maeneo mengi nchini kuna migogoro ya ardhi na baadhi yake imesababisha athari kubwa katika jamii ,vikiwemo vifo na kuharibiwa mali na wenyeji kufurushwa . Migogoro hii imekuwa ikitokea kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikitokana na vijiji vingi kutopimwa na kushindwa kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi . Mwanya huo wa kutopimwa vijiji umekuwa ukitumiwa vibaya na baadhi ya viongozi hasa wa kisiasa kwa kuwagawa wananchi kwa maslahi yao ya kisiasa . Migogoro hiyo ya ardhi tumeishuhudia ikipoa na kulipuka katika mkoa wa pwani mwa Kenya . Tumeshuhudia jinsi migogoro kadhaa ya wakulima na wafugaji ,waekezaji na wenyeji ambavyo imechangia vifo vya watu katika eneo bunge la Kinango ,kusini mwa pwani . Wadi ya Tiwi eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale ni miongoni mwa sehemu zinazoshuhudia migogoro ya ardhi , mabwenyenye wakionekana kujaribu kunyakua hata ardhi za misitu ya kaya . Nje ya mahakama ya Kwale nyuso za w...

HAJA YA MASHIRIKA YA KIJAMII KUSHIRIKIANA ILI KUENDELEZA MIRADI MASHINANI , ENEO LA MATUGA

Image
washirika wa mradi wa Participatory grant making Taarifa yake : Caroline Katana Mshirikishi wa mradi wa mpango wa pamoja wa kimikakati ya hatua za dini JISRA Kenya Zena Hassan , ametoa changamoto kwa makundi matano ya kijamii yaliyokuwa yakiendeleza miradi mbalimbali kwa jamii eneo la Matuga kaunti ya Kwale chini ya awamu ya pili ya mradi wa Participatory Grant Making (PGM2 ) kushirikiana kwa ukaribu na washika katika idara mbalimbali ili kuhakikisha uendelevu wa miradi hio . Hii ni baada ya mradi huo wa PGM 2 ulionza rasmi mwezi Machi mwaka huu kuingia kikomo mwishoni mwa mwezi huu wa saba kaunti ya Kwale ,awamu ya tatu ikitarajiwa kutekelezwa kaunti ya Isiolo kuanzia mwezi Agosti . Akizungumza na wanahabari baada ya kukamilika kwa mkao wa kutathmini miradi iliypkuwa ikitekelezwa na makundi hayo kilichowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Tiwi social hall ,bi Hassan amesisitiza umuhimu wa miradi hio kuendelezwa ili kutatua changamoto za kimsingi zinazo dumaza uk...

RAIS RUTO APONGEZWA KWALE HUKU ALI HASSAN JOHO NA SALIM MVURYA WAKITAKIWA KUEKA KANDO TOFAUTI ZA KISIASA.

Image
  wakaazi wa Kwale Taarifa yake : Caroline Katana  Wakaazi  kaunti ya Kwale sasa wanamtaka  waziri mteule Salim Mvurya na mwenzake  Ali Hassan Joho kueka  kando tofauti zao za kisiasa  na badala yake kushirikiana katika swala zima la kuhudumia taifa baada ya rais Wiliam  Ruto kuwateuwa katika wizara ya biashara  na uekezaji na ile ya madini na uchumi samawati  mtawalia . Kauli zao zinajiri baada ya rais Ruto kuvunja baraza la mawaziri  siku chache zilizopita  na kulifanyia mabadiliko ambapo  Salim Mvurya  ambae ameteuliwa kama waziri wa biashara na uekezaji aliishikilia wizara ya madini na uchumi samawati katika baraza lililopita. .Hamisi Juma Shomali Wakiongozwa na Hamisi Juma  Shomali  wameipongeza hatua ya rais Ruto kumrudisha katika wizara ,waziri Salim Mvurya ,wakiitaja hatua hio kuonyesha heshima kubwa kwa wakaazi wa Kwale na pwani nzima kwa ujumla . “Wakati baraza la mawaziri lilipovunjwa  sisi k...

CHAMA CHA UZALENDO CHA TISHIA KUJIONDOA KATIKA MUUNGANO WA AZIMIO

Image
wanachama wa CCU Taarifa yake ,Caroline Katana  Chama Cha Uzalendo  C C U  kimetishia kujiondoa katika muungano wa Azimio  na kujiunga na chama cha Wiper  ili kumpa nafasi kinara wa muungano huo Raila Odinga kujiunga na serikali ya Kenya Kwanza ili kuendeleza mazungumzo  ya kutatua changamoto msingi zinazolikumba taifa la Kenya  . Hii ni baada ya  chama  cha Uzalendo  kujitenga  na  mazungumzo  ya kitaifa  yanayopangwa na srikali  ya  Kenya  Kwanza  . Kinara wa  CCU   Richard Onsongo amesema kwamba kinara wa Azimio Raila Odinga anajipendekeza katika serikali ya Kenya Kwanza ili apate  kutengeza  nafasi za vyeo  katika serikali hio  swala ambalo hawaliungi mkono. . kinara wa chama cha ccu Kenya Richard Onsongo  Aidha amesema kwamba kuna haja ya rais Wiliam  Ruto  kubeba msalaba wake wenyewe katika maswala ya utatuzi wa changamoto zinazolikumba taifa ...

SHULE YA MSINGI YA WAA YANG’AA KIMAZINGIRA KUPITIA UFADHILI WA VYOO KUTOKA KWA KAMPUNI YA MOZZART BET KWA USHIRIKIANO NA WAKFU WA RASHID ABDALLAH .

Image
  Usimamizi wa kampuni ya Mozart bet pamoja na wadau mbalimbali. Wakfu wa  Rashid  Abdallah  umeukabidhi  rasmi  usmimamizi  wa shule ya msingi ya Waa  mradi wa vyoo  18, madawati 100, sodo miongoni mwa pembejeo zenginezo  za elimu ,  kupitia ufadhili wa kampuni ya ubashiri ya Mozatt bet  uliogharimu  takriban shilingi million 3.4. Hatua hio imejiri  kufuatia hali mbaya ya vyoo iliyokuwa ikishuhudiwa shuleni  humo iliyohofiwa kusababisha mikurupuko  ya maradhi yanayotokana na mazingira chafu. Mkurugenzi mkuu wa mozzart bet nchini Kenya  SaS'a  Krneta. Mk Mkurugenzi  wa kampuni hio ya Mozzart bet nchini kenya Sas’a Krneta amesema kwamba mazingira bora ya vyoo  utaimarisha hali ya usafi shuleni humo na kuhakikisha usalama wa kiafya kwa wanafunzi na walimu . “ Tumewakabidhi vyoo kumi na 18 ,saba  vitatumika na wanafunzi wakiume  vyengine saba  viwasaidia wanafunzi wakike huku ...