SEKTA YA UVUVI KWALE YAPIGWA JEKI
msafara wa naibu gavana na maafisa wa EU KEMFSED na waziri Kilimo, Uvuvi na ufugaji Taarifa yake : Caroline Katana Sekta ya uvuvi kaunti ya Kwale inatarajiwa kuimarika hata zaidi baada ya makundi ya wasimamizi wa bahari ( Beach Management Units ) kupokea boti nane za kisasa chini ya ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya EU kupitia mradi wa Go- Blue na serikali ya kaunti kupitia mradi wa KEMFSED . Boti tano zilizofadhiliwa na EU zitawafaidi wavuvi kutoka eneo la Shimoni , Kibuyuni na Mkwiro huko boti tatu za ulinzi ( patrol boats ) zilizofadhiliwa na serikali ya Kwale kupitia mradi wa KEMFSED zitatumika na wavuvi katika sehemu za ushirika za Shimoni –Vanga, Mwandamu- Funzi na Chale- Gazi. boti za Uvuvi kwale shimoni Zaidi ya wakaazi elfu kumi kusini mwa pwani wanategemea bahari moja kwa moja kujikimu kimaisha . Nchini kenya ,uvuvi unajumuisha Zaidi maji chumvi ( maziwa ,mito na mabw...